
BBC
imezindua huduma mpya ya umma ya kiteknolojia inayotoa taarifa za afya
kuhusiana na ugonjwa wa Ebola kupitia kwa programu ya kijamii ya kutuma
ujumbe mfupi kwenye internet ya 'WhatsApp.'
Programu hio inawalenga zaidi watumiaji wa Internet katika kanda ya Afrika Magharibi.
Huduma
hio itawezesha wasomaji kupata taarifa kwa njia ya sauti, ujumbe mfupi
na picha kuwasaidia kuepukana na maambukizi ya Ebola katika kanda nzima.

Taarifa zitakazopatiakana
kwenye App hiyo zitakuwa angalau tatu kwa siku na huduma yenyewe itakuwa
kwa lugha ya kiingereza na kifaransa.
Ili kupata taarifa kupitia kwa programu hiyo, tuma ujumbe mfupi...kupitia kwa WhatsApp kwa nambari +44 7702 348 651
WhatsApp
ndio programu inayotumiwa sana kwa kutuma ujumbe mfupi barani Afrika na
kwa kuitumia ina maana kuwa ujumbe huo utawafikia mamilioni ya watu
barani Afrika kupitia kwa simu zao za mkononi.
0 comments:
Post a Comment