
Mhudumu wa pili wa afya katika hospitali ya Texas ambapo maambukizi ya kwanza ya Ebola nchini Marekani yaligundulika amegundulika kuwa na ebola,serikali ya jimbo hilo imethibitisha Jumatatano(jana).
Kama ilivyokuwa kwa maambukizi ya awali,mgonjwa wa sasa ni mhudumu wa afya aliyemhudumia mgonjwa raia wa Liberia mwenye Ebola,ambaye baadae alifariki katika Hospitali ya Dallas, Idara yaHuduma za Afya ya Jimbo ilieleza.
Mhudumu wa pili alianza kuhisi ana homa siku ya jumanne na akalazimika mara moja hospitalini hapo.
"Madaktari wamemchunguza mgonjwa wa sasa ili kubaini muingiliano na hatari za maambukizi kwa watu alioshirikiana nao,na watu hao wazidi kuangaliwa",ilieleza taarifa hiyo.
Wauguzi wote wlimhudumia mwathirika wa Ebola Thomas Duncan,ambaye anaaminika kupata ugonjwa huo alipokuwa nchini Liberia.Thomas alifariki kwa ugonjwa huo tarehe 8/10/2014.
CHANZO: Daily Nation
0 comments:
Post a Comment