Tuesday, October 21, 2014

Tuesday, October 21, 2014


Oscar Pistorius akiwa kwenye gari tayari kupelekwa gerezani kuanza kutumikia kifungo chake


Mjomba wa Pistorius,Arnold Pistorius amesema familia imeumizwa na kuvurugwa kihisia na hukumu hiyo.


Gari lililombeba Oscar Pistorius kumpeleka gerezani likipita katikati ya waandishi wa habari na kundi la watu waliohudhuria hukumu hiyo.

Baada ya kutoshawishika na maombi ya timu ya utetezi ya kumpa mteja wao kifungo cha nje, leo Jaji Thokozile Masipa amemhukumu Oscar Pistorius kifungo cha miaka mitano gerezani.Jaji Masipa amemhukumu Pistorius kifungo kingine cha miaka mitatu kwa kosa la kufyatua bastola kwenye mgahawa mmoja huko Johanesburg Januari 2013,Adhabu hii imejumuishwa kwenye miaka mitano,ambayo inaanza mara moja.

Mwezi uliopita Pistorius alipatikana na hatia ya kuua bila kukusudia na kusababisha kifo cha mpenzi wake Reeva Steenkamp pamoja na kuptikana na hatia ya kutumia silaha kizembe katika tukio tofauti.

Jaji Masipa alisema kwenye hukumu hiyo alitumia majaji wengine wawili kumsaidia lakini uamuzi wa hukumu hiyo ulikuwa wake mwenyewe.

0 comments: