Shirika
la afya duniani WHO, linasema kuwa mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa Ebola
hautarajiwi kushuhudiwa katika mataifa Ulaya kwani nchi za Magharibi
zina mifumo thabiti ya afya kuweza kukabili ugonjwa huo.
Rais
Barack Obama wa Marekani pia amesema hatari kwa Wamarekani kupata virusi
vya Ebola ni ya "chini mno", ingawaje ameagiza"hatua thabiti
zichukuliwe" kukabiliana na ugonjwa huo. Marekani inachunguza
namna mtu aliyeambukizwa Ebola alivyoruhusiwa kusafiri kwenye ndege na
kumwambukiza muuguzi aliyekuwa akimtibu huko Texas.
Amber Vinson hakustahili kusafiri katika ndege, amesema afisa wa afya.
Maafisa wanajaribu kufuatilia watu 132 waliosafiri na Amber Vinson. Ugonjwa huo umeua watu wapatao 4,500 mpaka sasa, hususan katika nchi za Liberia, Guinea na Sierra Leone. Mawaziri
wa Afya wa Umoja wa Ulaya watakutana mjini Brussels Alhamisi kujadili
janga hili, ikiwemo uwezekano wa kupeleka askari zaidi huko Afrika
Magharibi kusaidia kudhibiti ugonjwa huo. Mkurugenzi wa mkakati wa
WHO, Christopher Dye, amesema kulipuka kwa Ebola nchini Marekani au
nchi nyingine Ulaya Magharibi ni jambo ambalo limeleta "wasiwasi
mkubwa".
Makumi ya watu waliokaribiana na mtu aliyekufa kutokana na Ebola nchini Marekani wanafuatiliwa afya zao.
"Uwezekano kwamba mara maambukizo yakitokea yanasambaa kwingineko, ni jambo ambalo kila mtu atakuwa na wasiwasi nalo, amesema. Lakini
ameongeza kusema: "lakini tuna uhakika kuwa Amerika Kaskazini na Ulaya
magharibi ambako mifumo ya afya ni imara sana, kwamba hatutarajii kuona
mlipuko mkubwa katika moja ya maeneo hayo." Mapema, Rais Obama
alisema uwezekano wa kusambaa kwa Ebola kwa kiasi hicho kama cha nchi za
Afrika magharibi ni "mdogo sana sana." Hata hivyo, ameahidi
"hatua thabiti zaidi" katika kufuatilia wagonjwa wa Ebola nchini
Marekani na amethibitisha mipango ya kupeleka"timu mkakati" ya wataalam
katika hospitali yoyote ambayo imeripoti maambukizo ya Ebola.
0 comments:
Post a Comment