Thursday, November 13, 2014

Thursday, November 13, 2014



MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA RUNGU KICHWANI WILAYA YA CHUNYA.
MTU MMOJA GASPER VISENTI [38], MKAZI WA KIJIJI CHA KALANGALI ALIKUTWA AMEUAWA PORINI BAADA YA KUPIGWA RUNGU KICHWANI NA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MOJA LA CLEMENT SIMKOKO @ YOHANA, MKAZI WA [W] MBOZI.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 12.11.2014 MAJIRA YA SAA 16:15HRS KATIKA KITONGOJI CHA IVUMWE, KIJIJI CHA KALANGALI, KATA YA MTANILA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA UKITOKA DAMU NYINGI PUANI NA MASIKIONI. CHANZO CHA TUKIO HILI NI KULIPIZA KISASI BAADA YA MAREHEMU KUMDHURUMU MTUHUMIWA PESA UJIRA WAKE BAADA YA KUMLIMIA SHAMBA LA TUMBAKU. HATA HIVYO MTUHUMIWA HUYO ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI AN AENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA PIA KUEPUKA MATATIZO YANAYOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAKE ZIWEZE KUCHUKULIWA MARA MOJA.
TUKIO LA PILI.
MTOTO MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA KUGONGWA NA PIKIPIKI WILAYA YA KYELA.
MTOTO MMOJA AITWAE MICHAEL MICHAEL [4], MKAZI WA NDANDALO ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI T.207 CUV AINA YA SUNLG ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA MOSE ANDREW [22],MKAZI WA NDANDALO.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 12.11.2014 MAJIRA YA SAA 12:30HRS KATIKA KIJIJI CHA NDANDALO, KATA YA KYELA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA, TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
TUKIO LA TATU.
WANAFUNZI WATATU WA KIKE WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI CHA UDONGO WILAYA YA ILEJE.
WANAFUNZI WATATU WA KIKE WANAOSOMA SHULE YA MSINGI ILOMBA AMBAO NI 1. SEVELINA MWILE [11], MKAZI WA KITONGOJI CHA ITALE 2. GRACE PATSON [10], MKAZI WA KITONGOJI CHA ITALE NA 3. AGEY SEME [10], MKAZI WA KITONGOJI CHA ILOMBA[W] MBEYA VIJIJINI WOTE WANAFUNZI WA DARASA LA NNE SHULENI HAPO WALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI CHA UDONGO WAKATI WAKICHIMBA UDONGO NDANI YA SHIMO.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 12.11.2014 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA ILOMBA, KATA YA ITALE,TARAFA YA BUNDALI WILAYA YA ILEJE MPAKANI NA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI,MKOA WA MBEYA. AWALI KABLA YA KUKUTWA NA MAUTI WAHANGA HAO WALICHUKULIWA SHULENI NA ISAMBI MWASENGA [57], MWALIMU MKUU MSAIDIZI WA S/MSINGI ILOMBA KWENDA KUMFANYIA KAZI BINAFSI YA KUCHIMBA UDONGO NA KUMPELEKEA NYUMBANI KWAKE. MIILI YA MAREHEMU IMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA YUPO MAHABUSU KWA AJILI YA USALAMA WAKE WAKATI UPELELEZI WA SHAURI HILI UKIENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUWATUMIKISHA KAZI WATOTO WENYE UMRI MDOGO KATIKA MAENEO/MAZINGIRA HATARISHI YATAKAYOWEZA KUSABABISHA MAAFA NA KUFANYA VITENDO VYA NAMNA HIYO NI KWENDA KINYUME CHA SHERIA.
Imesainiwa;
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

0 comments: