
Mamlaka nchini India zimebaini kuwa watu 430 wamekufa kutokana na wimbi la joto linalovuma nchini India.
Vifo vingi zaidi vimeripotiwa kwenye ukanda wa kusini miji ya Telangana na Andhra Pradesh, ambapo watu 140 wamepoteza maisha, tangu jumamosi wimbi hilo la joto lilipoanza.
Mji wa Allahabad ulioko Uttar Pradesh, umelisajili vipimo vya nyuzijoto 48C huku mji mkuu wa India ,New Delhi ukistahimili kiwango cha nyuzijoto 44C .
Viwango vya joto vimekuwa juu zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita lakini vifo vimeanza kuripotiwa mwishoni mwa juma.
Vifo vingi vimerekodiwa katika jimbo la Andhra Pradesh, ambapo jumla ya watu 246 wamethibitishwa kupoteza maisha kuanzia juma lililopita.
Kwingineko, chama cha waandishi wa habari kimesema kuwa watu 186 wamefariki katika wilaya 10 za jimbo la Telangana.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa imesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa hali hiyo ya joto kuendelea kwa siku kadha zijazo.
Waendesha teksi ambazo hazina kiyoyozi hawataruhusiwa kuhudumu kwa saa tano katika mji mkuu wa Kolkata, baada ya madereva wenzao wawili kufariki awali.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa inasema kuwa hali hiyo ya juu ya joto inatokana na ukosefu wa mvua.
0 comments:
Post a Comment