Wednesday, September 16, 2015

Wednesday, September 16, 2015

Rais Jakaya Kikwete leo amezindua jengo la kisasa la mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Uma (PSPF) na kuyataka mashirika mengine nchni kujenga majengo ya kisasa ili kuleta imani na matumaini kwa wawekezaji kuwa Tanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji.

Rais Kikwete amayasema hayo kwenye uzinduzi huo, na pia ameipongeza bodi ya wadhamini kwa kubuni wazo la kujenga jengo hilo. Amesema jengo hilo limebadili mandhari ya jiji la Dar es Salaam na ni alama inayoweza kuvutia na kujenga matumaini kwa wawekezaji wanaokuja nchni.

Naibu Waziri wa Fedha Mh. Adam Malima amesema ujenzi wa jengo hilo ni utekelezaji wa sera ya uwekezaji ambapo ameitaka PSPF kulitumia kama kitega uchumi ambapo pia,kupitia hafla hiyo, ameahidi kuwa serikali italipa madeni yote yanayodaiwa na mashirika ya hifadhi katika kipindi kifupi kijacho.

Mwenyekiti wa bodi ya wadhamani wa mfuko wa PSPF,George Yembesi amepongeza serikali ya awamu ya nne kwa kuhamasisha uwekezaji uliopelekea PSPF kubuni na kukamilisha ujenzi wa jengo hilo.

Aidha, Yambesi amesema kati ya changamoto kubwa zinazoikabili PSPF ni deni kubwa ambalo mfuko huo unalidai serikali na alitumia fursa hiyo kuomba lilipwe kabla ya kukamilika kwa uongozi wa serikali ya awamu ya nne.

Majengo pacha ya PSPF yana urefu wa mita 147 na ni jengo refu la kwanza katika nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki huku kwa bara la Afrika likiwa ni jengo la nane kwa urefu.

Mpaka kukamilika kwake jengo hilo limegharimu zaidi ya shilingi bilioni 139.2.

0 comments: