Thursday, September 17, 2015

Thursday, September 17, 2015

Serikali ya awamu ya tano iwapo itapewa ridhaa na watanzania imeahidi kuendelea kufungua milango ya kiuchumi kwa mikoa inayopakana na nchi jirani. Hayo yamesemwa leo Kigoma na mgombea urais kwa CCM Dkt. John Maguful huku pia akiwataka wakazi wa mipakani kulinda amani na mipaka ya nchi kwa kutoshiriki katika matukio ya kihalifu na kuweka mazingira mazuri ya kuvutia biasahara na nchi jirani na mkoa wa Kigoma.

Mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi ccm Dr John Pombe Magufuli ameyasema hayo kwa wananchi wa Kigoma ambao wanapakana na nchi jirani kadhaa kwa kuwataka kuilinda amani ya nchi na kuepuka vishawishi vya kushiriki katika matukio yanayohatarisha amani ya nchi pamoja na mali za watanzania ili Kigoma iweze kufunguka kiuchumi kwa kuwa na mazingira yanayovutia biasahara na nchi nyingine.
 
Pia Dr Magufuli ameahidi kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa mkoa wa Kigoma ikiwa ni pamoja na barabara, ukosefu wa maji lakini pia tatizo la usalama hasa wawapo safarini baada ya baadhi ya wananchi kuliibua ambapo baadhi ya magari ya abiria yamekuwa yakisindikizwa na askari polisi kutokana na hofu ya usalama.
 
Akiwa njiani akitokea Kigoma mjini kuelekea Kasulu na Kibondo,Dk Magufuli ambaye amekuwa akisimamishwa barabarani na wananchi ili aweze kusikiliza kero zao,amekuwa akiitumia fursa hiyo kuomba kura. Akiwa katika eneo la Kifura Dk Magufuli alielezwa na wananchi wa eneo hilo juu ya tatizo la barabara na hali ya ujambazi jambo linapelekea jeshi la polisi kusindikiza mabasi ya abiria na magari mengine hatua waliyodai kukamilika kwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutaondoa tatizo hilo.

0 comments: