Wednesday, October 15, 2014

Wednesday, October 15, 2014



Members of the media gather for a prayer vigil on the campus of TCU for health care worker Nina Pham who contracted the Ebola virus on October 14, 2014 in Dallas, Texas. The Texas Heath Presbyterian Hospital nurse contracted the virus while treating patient Thomas Eric Duncan, who has since died.   PHOTO | AFPWaandishi kutoka vyombo vya habari wakiwa wamekusanyika kwenye maombi kwa ajili ya Nina Pham, mhudumu wa afya katika Hospitali ya Presbyterian ambaye alipata maambukizi ya Ebola tarehe 14/10/2014 akiwa kazini hospitalini hapo.
Mhudumu wa pili wa afya katika hospitali ya Texas ambapo maambukizi ya kwanza ya Ebola nchini Marekani yaligundulika amegundulika kuwa na ebola,serikali ya jimbo hilo imethibitisha Jumatatano(jana).
Kama ilivyokuwa kwa maambukizi ya awali,mgonjwa wa sasa ni mhudumu wa afya aliyemhudumia mgonjwa raia wa Liberia mwenye Ebola,ambaye baadae alifariki katika Hospitali ya Dallas, Idara yaHuduma za Afya ya Jimbo ilieleza. 
Mhudumu wa pili alianza kuhisi ana homa siku ya jumanne na akalazimika mara moja hospitalini hapo.
"Madaktari wamemchunguza mgonjwa wa sasa ili kubaini muingiliano na hatari za maambukizi kwa watu alioshirikiana nao,na watu hao wazidi kuangaliwa",ilieleza taarifa hiyo.
Wauguzi wote wlimhudumia mwathirika wa Ebola Thomas Duncan,ambaye anaaminika kupata ugonjwa huo alipokuwa nchini Liberia.Thomas alifariki kwa ugonjwa huo tarehe 8/10/2014.
CHANZO: Daily Nation

0 comments: