Kiongozi mmoja katika jimbo la Borno alisema kuwa wapiganaji waliuwa wauza samaki karibu 50 karibu na kijiji cha Doron Baga, kando ya Ziwa Chad.
Alisema wapiganaji wa Boko Haram wameweka kizuizi kwenye njia ya kuelekea Chad na kuwakamata wachuuzi waliokuwa wakienda kununua samaki.
Katika tukio jengine hapo awali watu karibu 50 waliripotiwa kuwa waliuwawa karibu na mpaka wa Cameroon pale Boko Haram walipovamia kijiji cha Azara Kuya, siku ambapo soko huwa na watu wengi.