Kumetokea ajali mbaya mjini Mafinga eneo la Changalawe Mkoani Iringa baada ya abiria wanaodhaniwa kufikiwa 40 , wa basi la Majinja lilikuwa linatokea Mbeya kuelekea Dar es salaam kufunikwa na kontena.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mongi ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo.
Inasemekana idadi kubwa ya abiria hao wamefariki lakini Kamanda wa polisi mkoani Iringa, Bw.Mongi, akizungumza na vyombo vya habari kwa njia ya simu, amesema kuwa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo itatolewa mara baada ya kukamilisha zoezi la kuitoa miili katika gari hilo.
0 comments:
Post a Comment