Tuesday, March 24, 2015

Tuesday, March 24, 2015
Watu watano wamefariki dunia papo hapo katika kijiji cha Undomo wilayani Nzega mkoani Tabora baada ya magari manne kugongana usiku wa kuamkia leo.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Juma Bwire amethibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema haya:

"Ilikuwa ni gari ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega yenye namba SM 4905 ilikuwa na abiria watano,dereva na abiria wengine watatu ambao ni wafanya kazi wa TFDA walikuwa wanatokea Nzega Ndogo kwa ajili ya shughuli za mambo ya maduka",

"Walipofika eneo la Undomo gari hiyo ilikuwa inataka Kulipita gari jingine,ikaenda kugonga gari namba T654ACQ aina ya Pajero,kuna gari nyingine tena Toyota yenye namba T831ASK,ikaenda mbele zaidi ikagonga basi la Super Kenny namba T874CWD lililokuwa linatoka Mbeya kwenda Mwanza".

"Watu watano waliokuwa kwenye Landcruiser ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega wamefariki dunia,akiwemo dereva aliyejulikana kwa jina la Charles Sanga na afisa utumishi wa halmashauri hiyo Peter Stephen",alieleza Kamanda Bwire.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa basi lililohusika katika ajali hiyo lilipasuka tairi la mbele lakini dereva wake alijitahidi sana na matokeo yake abiria wake kujeruhiwa tu na hakuna aliyepoteza maisha katika basi hilo.

"Gari iliyosababisha ajali hiyo ni hiyo Landcruiser iliyokuwa imeenda kufanya ukaguzi pale Nata,walipomaliza kufanya ukaguzi waakaanza kunywa bia mbili tatu,kisha kuanza safari kuelekea Nzega,lakini walipofika kona ya Undomo gari likapoteza mwelekeo,basi lilipandilia gari hilo dogo,watu wote ndani ya gari dogo wakafariki dunia papo hapo", shuhuda wa tukio hilo Furaha Titus alieleza.

0 comments: