Sunday, March 29, 2015

Sunday, March 29, 2015
                         Lubitz
Mchumba wa zamani wa rubani aliyeangusha ndege ya Germanwings kwa makusudi katika milima ya Alps nchini Ufaransa, amenukuliwa na gazeti moja la Ujerumani akisema kuwa Andreas Lubitz alikuwa akipanga njama kubwa.


Mwanamke huyo, muandalizi katika ndege, ambaye alikutana na rubani huyo kazini mwaka jana, aliliambia gazeti la Bild kwamba rubani Lubitz alisema mara nyingi kwamba atafanya kitu ili kila mtu amkumbuke yeye ni nani.
Alimuelezea kuwa alikuwa mtu aliyekuwa akiteseka kichwani.
Mwandishi wa habari aliyemhoji dada huyo alikiri kwamba dada huyo alisema Lubitz alikuwa mtu mwema na hodari mbele ya watu, lakini faraghani alikuwa mkali hasa wakizungumzia kazi.
Anasema wakati mwengine anapata jinamizi na anaamka akipiga kelele "ndege inaanguka."
Anasema Lubitz alikasirika alipotambua hivi karibuni kwamba alikuwa hawezi kutimiza ndoto yake ya kuwa rubani kamili, kwa sababu ya ugonjwa wa akili.
Baada ya uhusiano wa siri baina yao kwa miezi mitano, dada huyo alijitenga na Lubitz kwa sababu ya hasira zake.

0 comments: