Huku nusu ya matokeo katika uchaguzi wa rais nchini Nigeria yakiwa yametangazwa hadi hivi sasa, mgombea kutoka chama kikuu cha upinzani, Muhammadu Buhari, anaongoza dhidi ya rais aliye madarakani, Goodluck Jonathan.
Lakini majimbo ya kusini yenye idadi kubwa ya watu kama vile Lagos na Rivers bado hayajatangaza matokeo na imebainika sasa kwamba katika mji mkuu Abuja mchuano bado ni mkali kati ya wagombea hao.
Tume ya uchaguzi imesema itaendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi Jumanne asubuhi na kwamba matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa baadaye siku hiyo. Yeyote atakayeshinda kati ya wawili, litakuwa jambo la kushangaza iwapo mgombea atakayeshindwa hatatamka kuwepo kwa mbinu chafu.
0 comments:
Post a Comment