Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Bi. Samia Suluhu Hassan wakionesha fomu za kugombea urais mara baada ya kukabidhiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam leo 04/08/2015.
Mh. Samia Suluhu Hassan akizungumza na halaiki iliyojitokeza kwa wingi nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya uchaguzi kuchukua fomu za kugombea urais leo asubuhi.
Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi wakiwa wamekusanyika nje ya Ofisi Ndogo ya Makao ya CCM mtaa Lumumba wakati Dkt John Pombe Magufuli akienda kuchukua fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),jijini Dar es Salaam leo.
0 comments:
Post a Comment