Mshambuliaji
mpya wa Arsenal aliyetokea kwenye klabu ya Manchester United, Danny
Welbeck jana usiku aliandika historia mpya katika michuano ya ligi ya
mabingwa wa ulaya. Akiitumikia klabu yake ya Arsenal kwa mara ya pili kwenye michuano
hiyo, Welbeck aliungana na washambuliaji Mike Newell, Andy Cole (mara
mbili), Alan Shearer, Owen (mara mbili) and Rooney – kuwa wachezaji
pekee raia wa Uingereza ambao wamewahi kufunga hat trick katika michuano
ya ulaya. Welbeck alianza kufunga magoli mawili katika kipindi cha kwanza kabla
ya Alexis Sanchez kuongeza la 3 na kuiwezesha Arsenal kwenda mapumziko
wakiwa mbele kwa magoli 3-0. Kipindi cha pili Welbeck alifunga goli la 4 – na kutimiza magoli
matatu kwenye mechi, ikiwa hat trick yake ya kwanza katika maisha yake
ya soka la ushindani. Burak aliifungia Galatasary goli la kufutia
machozi kwa mkwaju wa penati. Mpaka mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho Arsenal walikuwa wameshinda 4-1.
0 comments:
Post a Comment