
Mmoja wa majeruhi katika tukio hilo la moto akisimulia.



Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick, akiwa na mmoja wa wauguzi wa
hospitali ya Temeke alipowatembelea waathirika wa ajali hiyo. WATU
watatu wamefariki na wengine sita wakiwa katika hali mbaya Hospitali ya
Muhimbili kufuatia tukio la moto uliolipuka kwenye gari la kubeba mafuta
jana maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam.
AKizungumza
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna Mohammed
Mpinga, alisema ajali hiyo haikuleta athari yoyote baada ya gari lile
kupata ajali ila athari ilijitokeza baada ya watu kuvamia na kuanza
kuiba mafuta na baadaye kujaribu kuiba betri ndipo cheche za moto
zilipolipuka na kusababisha kuwaka kwa gari hilo.
Wakati
huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick, amewataka wananchi
kutokuwa na tabia ya kuvamia ama kuiba vitu pindi ajali zitokeapo.
Sadick alisema hayo alipotembelea hospitali ya Muhimbili na Temeke walipolazwa majeruhi hao.
0 comments:
Post a Comment