Emmanuel Okwi, wa pili kushoto akiifungia Simba bao la kwanza huku golikipa wa Polisi Moro, Abdul Ibad akiuangalia mpira ukijaa wavuni.
Timu ya soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam imelazimishwa sare na timu ya Polisi Morogoro katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa taifa leo.
Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata goli katika dakika 32 kupitia kwa Mganda Emmanuel Okwi na goli hilo kudumu hadi mapumziko,
Aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa Simba, Danny Mrwanda, aliisawazishia Polisi baada ya kumzidi mbio na maarifa mlinzi wa Simba,Joseph Owino, na kabla ya kumchambua vizuri kipa wa Simba Hussein Sharrif 'Cassilas'.
Hii inakuwa ni sare ya pili mfululizo kwa Simba inayonolewa na Mzambia Patrick Phiri, baada ya wiki iliyopita kutoka 2 - 2 na Coastal Union.
Michezo mingine ya Ligi Kuu iliyopigwa leo imeshududia Azam FC ikiibuka ikiifunga Ruvu Shooting 2 - 0. Mtibwa Sugar wameifunga Ndanda FC 3 - 0. Coastal Union imeshinda 1 - 0 dhidi ya Mbeya City na Stand United ikiifunga Mgambo Shooting 1 - 0.
0 comments:
Post a Comment