MCHUNGAJI Peter Rashid
Abubakari wa Kanisa la RGC lililoko Mbezi ya Shamba jijini Dar, amedaiwa
kuoa mke wa pili aitwaye Pamela Didas Asenga akiwa na umri wa miaka 20
tu ‘dogodogo’.
Kwa mujibu wa chanzo, ndoa hiyo ilifungishwa na Askofu Innocent
Lugagi wa Kanisa la White House la Durban, Afrika Kusini, Agosti 29,
mwaka huu.
Mke mwingine wa mtumishi huyo wa Mungu anaitwa Zuwena (Catherine)
aliyemuoa mwaka 1985. Lakini kuna madai kwamba, mke huyo amemwacha.
Chanzo chetu ndani ya kanisa hilo kilidai kwamba, mchungaji huyo
aliwaambia waumini wake aliamua kumuoa Pamela kwa vile ndoa yake ya
mwanzo aliifunga akiwa Muislam na alifungishwa na shehe (hakumtaja
jina).
“Alituambia Mungu amemfunulia na amempa mke mwingine mwema ambaye ni binti mbichi, watu wewee,” kilisema chanzo.
Habari zaidi zinasema kuwa, mchungaji huyo baada ya kutua nchini,
Jumapili moja akiwa kanisani kwake aliwatangazia waumini wake, hasa
wanaume kwamba kama wana wake ambao walichukuana wakati wa ‘ujinga’ na
wamekaa nao kwa miaka mitatu au zaidi na hawana tabia ya Kimungu,
mkorofi na mchokozi na hawajafunga nao ndoa, wawaache ili Mungu awape
wake wema.
Sasa baada ya picha za mtumishi huyo kusambaa hadi kwenye mitandao, Risasi , juzi lilifika kanisani kwake Mbezi ili kuzungumza naye lakini hakuwepo.
Sasa baada ya picha za mtumishi huyo kusambaa hadi kwenye mitandao, Risasi , juzi lilifika kanisani kwake Mbezi ili kuzungumza naye lakini hakuwepo.
Baadhi ya waumini walioweza kuzungumza na Risasi walionesha
kushtushwa na kitendo cha mchungaji wao kumuoa Pamela lakini hawakuwa
tayari kusema neno!
Baadaye mwandishi wetu alimtafuta mchungaji huyo kwa njia ya simu ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Nipo Kiluvya kikazi lakini hilo lipo ila ni jambo langu binafsi siyo la kulitangaza.”
Baadaye alimtumia ujumbe mwandishi akiwa ameuandika hivi:
“Sanchawa mimi ni Nabii wa Mungu Yehova, uliponipigia tu kila kitu Mungu akaniambia nia yako na kusudi lako.”
Baadaye alimtumia ujumbe mwandishi akiwa ameuandika hivi:
“Sanchawa mimi ni Nabii wa Mungu Yehova, uliponipigia tu kila kitu Mungu akaniambia nia yako na kusudi lako.”
Pia Risasi lilizungumza na baadhi ya wachungaji wa makanisa
ya kiroho Tanzania ili kuwasikia wanasemaje kuhusu kitendo cha mtumishi
huyo kufunga ndoa nyingine.
0 comments:
Post a Comment