Majaji wa mahakama ya jinai ya ICC wameamua kuwa rais wa Kenya hana budi ila kufika mahakamani binafsi Oktoba tarehe 8.Majaji
hao wamekatalia mbali ombi la mawakali wa rais Uhuru Kenyatta la kutaka
aruhusiwe kuhudhuria kikao hicho kupitia kwa njia ya Video ama kikao
hicho cha ana kwa ana kiahirishwe hadi siku nyingine kwani alikuwa
amekabwa na kazi na majukumu kama rais wa Kenya.
Majaji hao wanasema kuwa Rais Uhuru Kenyatta hakutoa sababu madhubuti ya kukosa kuhudhuria kikao hicho maalum.
Majaji
hao aidha wanasema kuwa Bwana Kenyatta lazima awe hapo ilikujibu
maswali muhumi kuhusu ushirikiano wa serikali yake na kujadili maswala
muhimu yatakayojadiliwa katika kikao hicho.
Kenyatta alikuwa ameiamboa mahakama kuwa ameratibiwa kuhudhuria sherehe za kuadhimisha uhuru wa Uganda .
Kauli
hiyo inawadia wakati ambapo mwendesha mashataka wa mahakama hiyo Fatou
Bensouda alikuwa amepinga ombi la rais Kenyatta la kuahirisha kikao
hicho ama kuruhusiwa kushiriki kikao hicho kwa njia ya video.
Bi
Bensouda alikuwa ameilalamikia mahakama hiyo akidai kukosa ushahidi wa
kutosha baada ya serikali ya Bw Kenyatta kumnyima stakabadhi alizotaka
ilikuimarisha kesi dhidi ya kiongozi huyo wa Kenya.
Bw Kenyatta
kwa upande wake naye alikuwa amewasilisha ombi mahakamani ya kutaka kesi
dhidi yake itupiliwe mbali baada ya bi Bensouda kukiri kuwa hakuwa na
ushahidi wa kutosha dhidi yake.
0 comments:
Post a Comment