Mgonjwa
wa kwanza wa ugonjwa hatari wa virusi vya Ebola amegundulika nchini
Marekani, imethibitishwa katika mji wa Dallas, Texas.
Maafisa
katika kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian
wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa ametengwa katika hospitali hiyo.
Mgonjwa
huyo anasemekana kuwa ni mtu anayeaminika kuambukizwa ugonjwa huo
nchini Liberia kabla ya kuonyesha dalili za ugonjwa huo.
Zaidi ya
watu 3,000 tayari wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola huko
Afrika Magharibi na idadi ndogo ya wafanyakazi wa Marekani wa mashirika
ya misaada wamepata nafuu baada ya kupelekwa kutibiwa Marekani.
Jumatatu,
maafisa wa kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian ya
Dallas wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa jina alikuwa akichunguzwa
virusi vya Ebola na ametengwa katika hospitali hiyo.
Shirika la
Afya Duniani, WHO limesema mpaka sasa zaidi ya watu 3,000 wamekufa
kutokana na virusi vya Ebola, wengi wa waliokufa ni kutoka Liberia.
Nchini
Nigeria, nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika kuna wagonjwa 19
waliothibitika kuugua ugonjwa wa Ebola na watu wanane wamekufa tangu
mgonjwa wa kwanza kuthibitishwa nchini humo mwezi Julai..
Kuna mgonjwa mmoja aliyethibitika nchini Senegal, lakini hakuna taarifa za kifo mpaka sasa.
Ebola ni ugonjwa hatari wa virusi kuwahi kuzuka duniani.
CHANZO: BBC
0 comments:
Post a Comment