Mkuu
wa huduma za Kibenki kwa Wafanyabiashara wakubwa wa Benki ya NMB,
Filbert Mponzi (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya
shilingi Milioni 19.4 kwa Rais wa Golf Tanzania, Joseph Tango jana
kwaajili ya mashindano Nyerere. Anaeshuhudia ni Kaimu nahodha wa Klabu
ya Golf ya Dar es Salaam, Shakil Jaffer.
BENKI ya NMB imetoa Sh.milioni 19.4 kwa ajili ya kudhamini mashindano ya Gofu ya taifa yajulikanayo kama ‘Nyerere Master Tournament’ yatakayo fanyika Jumamosi na Jumapili kwenye viwanja vya Gymkhana Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Gofu Tanzania Joseph Tango alisema zaidi ya wachezaji 100,kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara wanatarajia kushiriki mashindano hayo ambayo yupia yatashirikisha wachezaji warika tofauti tofauti.
Tango alisema katika mashindano ya mwaka huu watatumia matundu 30 siku ya kwanza wakitumia mashimo 18 na siku ya pili nay a mwisho watatumia tena mashimo 18 na kukamilisha idadi hiyo ambayo kitaalamu inakidhi haja kutokana na wingi wa klabu zinazo shiriki.
“Tunawashukuru NMB,kwa kuendelea kudhamani mashindano yetu kwa mwaka watatu sasa na kitu cha kufuraisha nikwamba zawadi kwa mwaka huu zimezidi kuongezeka katika kila umri na mashindan haya yanafaida kubwa kwa taifa kubwa ikiwa ni kusaidia kupata wachezaji wa timu za taifa,”alisema Tango.
Kwaupande wake Filbert Mponzi kutoka NMB ambaye ni Mkuu wa Huduma za Kibenk kwa Makampuni Makubwa,alisema dhamira yao ya kuendelea kudhamini mashindano hayo ni kutokana na heshima a kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere.
Alisema kitu kingine kinacho wasukuma kuendelea kudhamini mashindano hayo ya Gofu kwa mwaka wa tatu mfululizo ni lengo lao la kuendeleza michezo na kulitangaza taifa katika anga za kimataifa
“Tunawaomba wanachi wajitokeze kwa wingi Jumamosi na Jumapili kuja kushuhudia mashindano haya ambayo kiukweli yanaushindani mkubwa tofauti na watu wanavyofikiria,”alisema Mponzi.
Naye nahodha wa Gymkhana klabu Shakili Jaffer,aliishukuru NMB kwa kufanikisha mashindano hayo kufanyika Dar es Salaam na amewahakikishia mashabiki wao watapambana na kuibuka mapingwa dhidi ya wapinzani wao kutoka mikoani.
Mikoa ambayo itashiriki mashindano hayo ni pamoja na Morogoro Lugalo,Arusha,Manyara na Misenye na klabu zote tayari zimeshawasili Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano hayo.
0 comments:
Post a Comment