Mkurugenzi wa Kampuni yaLino Agency,waandaaji wa Miss Tanzania, HashimLundenga
Mashindano la Miss Tanzania 2014 yaliyokuwa lifanyike Jumamosi sasa halitafanyika hadi pale kesi ya msingi iliyozua mzozo baina ya wakurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency inayoratibu mashindano hayo itakapomalizika.
Jana, mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Dar es
Salaam ilitupa pingamizi la muda lililowasilishwa na mwanzilishi wa
mashindano hayo, Hashim Lundenga akipinga maombi ya zuio la muda la
kusimamisha mashindano yaliyotarajia kufanyika Jumamosi lilowasilishwa
na mshirika wake, Prashant Patel.
Uamuzi huo ulitolewa jana na hakimu mkazi wa
mahakama hiyo, Frank Moshi baada ya kusikiliza pingamizi hilo la awali
lililowasilishwa na Lundenga kupitia wakili wake, Audax Kahendaguza.
Lundenga kupitia wakili wake aliwasilisha
pingamizi hilo juzi akipinga maombi hayo yaliyowasilishwa na Patel
ambaye ni mwanzilishi mwenza wa mashindano hayo pamoja na Lundenga.
Katika maombi ya Patel, aliiomba mahakama hiyo
kutoa zuio la muda kwa mashindano hayo lililotarajia kufanyika katika
Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Patel kupitia kwa wakili wake, Benjamin Mwakagamba
aliiomba mahakama hiyo itoe zuio hilo ili kusubiri uamuzi wa kesi ya
msingi aliyoifungua mahakamani hapo dhidi ya Lundenga. Katika pingamizi
la awali, Lundenga alidai mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa amri hiyo
inayoombwa, hati ya kiapo inayounga mkono maombi hayo ina upungufu, pia
maombi yameletwa kabla ya muda.
Katika uamuzi wake, hakimu Moshi alikubaliana na
hoja za wakili wa Patel, Mwakagamba kwamba mahakama yake ina mamlaka ya
kusikiliza maombi ya zuio na kwamba yameletwa chini ya vifungu
vinavyostahili.
Wakati wa usikilizwaji wa pingamizi hilo, wakili
wa Lundenga alidai kwamba Patel amefungua kesi ya msingi kuhusu fedha na
siyo mashindano hayo. Alidai katika hati ya makubaliano, walikubaliana
kwamba siku tano kabla ya mashindano, mteja wake (Lundenga) angetakiwa
kumpatia mshirika wake, Patel Sh12 milioni.
“Mheshimiwa, mdai kafungua kesi ya msingi Septemba
29, ikiwa ni siku 12 kabla ya mashindano na maombi ya zuio ameyaleta
Oktoba 3, ikiwa ni siku nane kabla ya mashindano hayo. Hivyo, alitakiwa
kusubiri kuona kama hatalipa au la,” alidai wakili huyo.
Mashindao ya Miss Tanzania yalirejeshwa rasmi 1994
baada ya kuzuiwa na Serikali na yamekuwa yakiratibiwa na Lino Agency
ambayo yanamilikiwa kwa pamoja.
Mshindi wa mwaka jana, Happiness Watimanywa atalazimika kuendelea kusubiri kwa muda ili kumpata mrithi wake.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment