Friday, July 24, 2015

Friday, July 24, 2015


Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) , inatarajia kufunga kamera 400 za CCTV pamoja na mashine 3 za utambuzi wa mizigo, ikiwa ni njia mojawapo ya kuimarisha ulinzi katika  bandari ya Dar es Salaam.
 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Awadh Massawe ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi hundi ya shilingi milioni mbili kwa Taasisi ya Habari Development Association ili kuandaa mafunzo ya kuwawezesha waandishi wa habari kujenga weledi wa kufanya tafiti na kuandika habari za kupambana na ujangili.
 
Amesema bandari ya Dar es Salaam ni sehemu ya mpaka wa taifa, hivyo lazima TPA iunge mkono kuelimisha jamii  bila kufanya hivyo hakutakuwa na utalii na kulikosesha taifa mapato.
 
Mkurugenzi wa Habari Development Association,Bw. Kunze Mswanyama amesema waandishi wa habari wanahitaji kujenga weledi zaidi wa kupambana na ujangili wa rasirimali za nchi ili taifa liweze kunufaika nazo.
 
Taasisi hiyo inaundwa na waandishi wa habari wanaoandika habari za kupambana na ujangili na rasilimali katika Mbunga mbalimbali zikiwemo za Sadani, Serengeti, Mikumi na Selous.

0 comments: