Tuesday, March 17, 2015

Tuesday, March 17, 2015
                              ak47
Mdogo wa mwanamuziki Jose Chameleone, AK47,ambaye pia ni mwanamuziki amefariki dunia jana usiku kwenye baa ya Dejavu,Kansanga - Uganda.

Msanii huyo alijipatia umaarufu kwa kibao chake cha ‘Gimme Di AK’ alitereza na kuanguka alipoenda chooni kwenye baa hiyo na baadae aliaga dunia njiani akiwa anapelekwa hospitali ya Nsambya.
“Hii ni habari mbaya kuwahi kuwahi kutokea. Nimeambiwa na meneja wa Leon Island kwamba mdogo wetu A.K 47 amefariki...RIP” the self proclaimed Big Size, Bebe Cool aliandika kwenye mtandao.


Eddy Kenzo nae pia aliandika: “Rest in peace Ak47 bambi nze kyimpeddeko banange Oh God.”

WASIFU WAKE

AK47 alikuwa muimbaji wa dancehall musician, aliyezaliwa na kukulia kwenye familia ya kimuziki ikiongozwa na baba yao Gerald Mayanja na mkewe Prossy Musoke. Aliibuka kimuziki na singo yake “Gimme Di AK” baada ya kupikwa na kaka yake, Jose Chameleone kwenye majukwaa na matamasha mbalimbali.
Alikuwa kati ya wanamuziki wachanga wenye vipaji vinavyokuwa kwenye muziki nchini Uganda. AK47 alipata tuzo ya "best new HiPipo Charts artist" mwaka 2012 na akapata tena tuzo za Buzz Teeniez awards mwaka 2013. AK 47 alikuwa ni mdogo wa wanamuziki watatu: Dr Jose Chameleone, Weasel na Pallaso.

0 comments: