Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress akisisitiza jambo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya uongozi bora kwa vijana yaliyoanzishwa na Rais wa Marekani, Barrack Obama kupitia taasisi ya Mandela Fellowship, Ohio University na Institute for International Journalism.
Mkurugenzi wa mafunzo ya Yali Connect Camp, Dk Yusuf Kalyango akizungumza na wahitimu 18 wa mafunzo hayo.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mh Joshua Nassari akipozi katika picha na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress mara baada ya kukabidhiwa cheti cha uhitimu.
Vijana kutoka mataifa manne wakimsikiliza Balozi wa Marekani nchini Tanzania (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi bora kwa viongozi vijana wa baadaye yaiyomalizika hivi karibuni jijini.
Jumla ya vijana 18 kutoka nchi za Kenya, Uganda, Mauritius, Seychelles na Tanzania wemehitimu mafunzo ya wiki mbili ya uongozi bora yaliyoanzishwa na Rais wa Marekani, Barrack Obama.
Mafunzo hayo yaliendeshwa nchini chini ya programu ya Connect Camp chini ya Mandela Washington Fellowship, Chuo Kikuu cha Ohio na Taasisi ya Kimataifa ya Uandishi wa Habari (Institute for International Journalism) yenye malengo ya kuwapa uwezo vijana wa kuwa viongozi bora wa baadaye.
Akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo, Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress aliwataka vijana hao kutumia mafunzo hayo kwa mafanufaa katika fani zao na nchi husika kwani ni nyenzo ya kuwa viongozi bora wa baadaye hapa duniani.
Childress alisema kuwa Rais Obama ameanzisha mafunzo hayo kutokana na kutambua umuhimu wa uongozi bora na kuamini kuwa vijana ndiyo taifa la kesho.
“Nimefurahishwa na mwamko wa mafunzo haya, nawaomba myatumie kwa ajili ya maendeleo yenu na kwa nchi husika, hii ni nyenzo pekee katika kufikia lengo mlilojiwekea,” alisema Childress.
Mafunzo hayo yanayojuliana kwa jina la ‘Young African Leadership Initiative (Yali) yalishirikisha vijana nane (8) wa Kitanzania, wanne Uganda, huku Kenya, Mauritius na Seychelles zikiwakilishwa na watu wawili wawili.
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo ni Mbunge wa Chadema jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nasari ambaye alisema atatumia mafunzo hayo kujihimarisha kisiasa na kushinda kiti ha ubunge katika jimbo hilo.
0 comments:
Post a Comment