Friday, July 24, 2015

Friday, July 24, 2015


Wakati matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Burundi yanatarajiwa kutangazwa wakati wowote, kiongozi wa upinzani nchini humo amemtolea wito Rais Pierre Nkurunziza kukubali pendekezo la kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Wito huo umetolewa na kiongozi wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa ambaye amemtaka Rais Pierre Nkurunziza, kuitisha mazungumzo na wapinzani na kuunda serikali ya muungano wa kitaifa k
ufuatia uchaguzi wenye utata. 

Upinzani umekuwa ukimlaumu Rais Nkurunziza kukiuka katiba kwa kugombea muhula wa tatu madarakani, na hivyo kususia uchaguzi huo uliofanyika mapema wiki hii ambao unampa nafasi kubwa Bw. Nkurunzira kushinda.

Wakati huo huo wataalam wa Umoja wa Afrika wameanza kupelekwa nchini Burundi kwa lengo la kuchunguza na kusimamia zoezi la kuwapokonya silaha raia wanao zimiliki kinyume cha sheria na kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu.

Awali Marekani iliishutumu serikali ya Burundi kwa kujaribu kuzuia kupelekwa kwa wataalam hao kabla ya uchaguzi wa urais uliofanyika Julai 21.

0 comments: