Friday, July 24, 2015

Friday, July 24, 2015


Kaya zipatazo 260 za waathirika wa mafuriko wanaoishi kwenye mahema katika eneo la Mateteni wilayani Kilosa mkoani Morogoro zinaishi maisha magumu kwa kutegema viazi vitamu na nyingine hulazimika kulala nje na familia zao kutokana na uchakavu wa mahema.
.
Wahanga hao wamelalamikia kuendelea kuishi maisha magumu kutokana na uchakavu wa mahema ambapo baadhi yao wanalala nje na watoto na kuishi kwa kutegemea viazi vitamu kusukuma maisha ambapo wameomba serikali kuwaonea huruma kutokana na maisha magumu wanayoishi.

Nae mtafiti kutoka taasisi ya Naliendele  Bi.Bernadeta Kimata akizungumza na wananchi hao amesema waliliona hilo na ndio maana wakagawa mbegu za viazi bure kwa wananchi ili kuwezesha waathirika hao kupata chakula kwa muda mfupi kitakachowawezesha kukabiliana tatizo la njaa ambapo amewataka walime viazi kwa wingi viwasaidie kupunguza ugumu wa maisha na hasa tatizo la uhaba wa chakula linalowakabili kwa sasa.

Chanzo: ITV

0 comments: