Saturday, May 23, 2015

Saturday, May 23, 2015
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi  Rais Jakaya Kikwete amewataka viongozi wa CCM kuweka tofauti zao pembeni na kuhakikisha wanapitisha majina ya wagombea wenye sifa na wanaokubalika na wananchi kwenye uchaguzi mkuu ujao ili chama hicho kiweze kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu ujao..

Angalizo hilo limetolewa wakati akifungua mkutano mkuu wa halmashauri kuu ya CCM {NEC} ambapo ameonya endapo viongozi wa chama hicho watapitisha majina ya wagombea kwa utashi wao, na kusahau kuwa nguvu kubwa ya ushindi hutoka kwa wananchi ambao ndio wengi basi chama kisitarajie kuibuka na ushindi mkubwa kama ilivyokuwa kwenye chaguzi za miaka ya nyuma.
Kabla ya Rais Kikwete kufungua mkutano wa halmashauri kuu (NEC) kamati kuu ya CCM ilikuwa imefanya tathmini ya mwenendo wa mchakato zoezi la upigaji wa kura ya maoni ya katiba mpya na kuitaka serikali kujadiliana  na tume ya taifa ya uchaguzi NEC,na kuangalia namna ya kutatua changamoto zinazolikabili zoezi hilo ambazo zinaweza kuwa kikwazo kwa kura hiyo kwenda sambamba na uchaguzi mkuu ujao kama ilivyotangazwa awali.
Kamati hiyo ambayo inalazimika kukaa kwa siku mbili mfululizo kinyume na ratiba iliyotolewa awali ya siku moja na kutoa ushauri huo baada ya kupitia hoja mbalimbali ambapo,pamoja na mambo mengine imebaini zoezi la upigaji kura ya maoni ya katiba mpya linakbiliwa na changamoto lukuki zikiwemo kasi ndogo ya uandikishaji wa daftari la kudumu.
Changamoto zingine zilizobainishwa kuikabili kura hiyo ni pamoja na matakwa ya kisheria ambayo yanaelekeza zoezi hilo liende pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi kwa siku 60 siku 30 za kampeni na baada ya hapo ndipo ipegwe kura ya maoni ambapo tathmini inaonyesha hakutakuwepo na muda wa kutosha kabla ya tarehe 25 October inayotajwa kuwa ndio tarehe rasmi ya uchaguzi mkuu.

0 comments: