Saturday, May 23, 2015

Saturday, May 23, 2015
                       
Mkufunzi wa klabu ya Napoli ya nchini Italia, Rafael Benitez (pichani) ameorodheshwa miongoni mwa makocha wanaotarajiwa kumrithi Carlo Ancelotti katika klabu ya Real Madrid.

Ancelotti anatarajiwa na wengi kuachana na kilabu hiyo baada ya mechi ya mwisho na Getafe wikiendi hii.Hatua hii inatarajiwa kutokana na mwenendo mbaya ambao klabu hiyo imekuwa nao kwa baadhi ya mechi za hivi karibuni.

Mazungumzo kati ya Real Madrid na Benitez yanaendelea huku mkatabaa wa Benitez katika klabu ya Napoli ukitarajiwa kukamilika mwezi ujao, na mpaka sasa hapajakuwa na mazungumzo au makubaliano yalioafikiwa kuongeza mkataba huo.

Klabu ya West Ham pia inatajwa kuwasiliana na kocha huyo ambaye aliwahi kuzifundisha timu za Chelsea na Liverpool, zote za uingereza.

Benitez ambaye alianza kazi ya ukocha kwenye kikosi cha pili cha timu ya Real Madrid, amewahi pia kufundisha timu za Valladolid, Osasuna, Etramadura, TenerifeValencia na Inter Milan.

0 comments: