Thursday, April 16, 2015

Thursday, April 16, 2015
Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta akionyesha baadhi ya Ripoti za uchunguzi za Mamlaka ya Bandari,TPA na Ripoti ya shirika la Reli (TRL)jijini Dar es Salaam leo.Waziri Sitta amezungumza na waandishi wa habari leo kuelezea hatua 
alizochukua dhidi ya watendaji wa TRL.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli nchini(TRL),Mhandisi Kapallo Kisamfu amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa malipo ya Sh. Bilioni 230 ya mabehewa ya Mizigo yenye kasoro pamoja na kufanya malipo ya mabehewa yote kabla ya kukamilika.

Akitangaza maamuzi hayo ya kusimimishwa kwa Mkurugenzi huyo leo jijini Dar es Salaam baada ya ripoti ya kamati iliyoundwa na Waziri wa Uchukuzi (ambaye sasa ni Waziri wa Afrika Mashariki), Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta amesema ameshtushwa na malipo hayo kwani yamekiuka manunuzi ya umma kwani mkataba wake ulikuwa TRL ilipe nusu ya asilimia 50 lakini matokeo yake mabehewa yamelipwa yote.

Amesema mabehewa 120 yaliyofika nchini yakiwa yana kasoro aliyazuia baada ya kubaini hivyo lakini TRL ilikuwa imeshalipa fedha yote katika mazingira hayo yanaonyesha mkataba una dalili ya hujuma.

Waliosimamishwa wengine ni Mhandisi Mkuu wa Mitambo TRL,Ngosomwile Ngosomiles,Mhasibu Mkuu,Mbaraka Mchopa ,Mkaguzi Mkuu wa Ndani Jasper Kisiraga pamoja na Meneja Mkuu Ferdinand Soka.

Kamati ya uchunguzi kwa watendaji hao kwa kuidhinishwa kwa kulipwa kwa mabilioni ya Shilingi itaongozwa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru),Mamlaka ya udhibiti wa Ununuzi katika sekta ya Umma (PPRA),pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

0 comments: