Thursday, April 16, 2015

Thursday, April 16, 2015
              Basi likiwa linasombwa na maji ya mafuriko

Maafisa wa shirika la Msalaba Mwekundu kwenye mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya wanasema kuwa takriban watu 16 wametoweka baada ya basi kusombwa na mafuriko kilomita chache kutoka mji huo.


Mvua kubwa iliripotiwa kunyesha katika eneo la mji huo na viunga vyake mapema Alhamisi.

Katibu Mkuu wa shirika la Msalaba mMekundu Abbas Gulet anasema kuwa wamewaokoa watu 42 mpaka sasa.

Basi hilo liliondoka mjini Mandera kuelekea jijini Nairobi mapema siku ya jumatatu kabla ya kukwama katika matope.

Baadaye mvua kubwa ilinyesha na mafuriko kulisomba basi hilo.

Maafisa wa msalaba mwekundu wanasema kuwa wameanza kuwasaka watu waliotoweka katika mto mmoja ambao maji ya mafuriko hayo yanaelekea.

0 comments: