Thursday, April 16, 2015

Thursday, April 16, 2015
 Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe akiwahutubia wananchi Manyoni Mjini.
 Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Bi.Anna Mghwira, akiwahutubia wakazi wa Wilaya ya Manyoni .

 Viongozi mbalimbali wa ACT wakiimba wimbo wa taifa.
Zitto akizungumza na wakazi wa Mji wa Singida leo.

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema kinaweza kuunganisha nguvu na vyama vingine vya upinzani ili kukiondoa chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu ujao ambapo alisema shauku kubwa ya wananchi ni kutaka kujua msimamo wa ACT Wazalendo katika kushirikiana na vyama vingine vya siasa ili kufanikisha malengo ya kuiondoa CCM katika madaraka.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Singida na Kiongozi wa ACT wazalendo Zitto Kabwe wakati akihutubia mamia ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi ukombozi.

"Tumedhamiria kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kuubomoa mfumo  unaonyonya wananchi. Msimamo wetu upo wazi na tumeueleza mara kadhaa"alisema na kuongeza

“ACT- Wazalendo tunaunga mkono juhudi zozote za kushirikiana kwa vyama na hili linathibitishwa na jina letu Alliance na msimamo wetu kuhusu mabadiliko ya Katiba. Kubwa tunataka ushirikiano utakaonufaisha wananchi na sio ushirikiano wa kugawana nafasi za uongozi,” alisema Zitto.

Kiongozi huyo wa ACT alisema chama hicho hakina tatizo na kipo tayari kushirikiana na chama chochote kilichokuwa  tayari kushirikiana nao ikiwemo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Alisema umoja huo ni lazima uwe na malengo ya kujenga uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora, wenye mfumo wa hifadhi ya jamii kwa wananchi wote na wenye kutokomeza umasikini.

Alikanusha chama hicho kutoa  kauli yeyote dhidi ya UKAWA kama inavyoaminishwa na baadhi ya watu, bali wameweka wazi kuwa lazima misingi ya kiitikadi na kifalsafa izingatiwe katika ushirikiano wowote.

0 comments: