Mkuu wa kampuni ya Apple Tim Cook ametangaza jinsia yake akisema kuwa ''anajivunia kuwa shoga''..
Bwana Cook alitoa tamko hilo ili kujaribu kuwasaidia watu wanaong'ang'ana kutangaza jinsia zao katika ripoti iliochapishwa katika gazeti la biashara la kila wiki la Bloomberg.
Amekuwa wazi kuhusu jinsia yake,lakini pia amejaribu kuweka maisha yake katika faragha hadi sasa alisema.
Wiki hii Bwana Cook alitoa changamoto kwa jimbo lake la Alabama kuhakikisha kuwa haki za mashoga na wale wanaobadili jinsia zinaheshimiwa.
''Mimi sijitambui kama mwanaharakati,lakini nimegundua nilivyofaidika na mikakati iliowekwa na wengine'',alisema bwana Cook.
''Kwa hivyo iwapo watu wakisikia kwamba mimi ni shoga kutawasaidia baadhi yao ,ama kumpa faraja yule anayejisikia mpweke ama kuwashinikiza wengine kupigania haki zao,basi afadhali kutangaza maisha yangu ya faragha''aliongezea.
Bwana Cook amesema amekuwa wazi kuhusu jinsia yake na watu wengi wakiwemo wafanyikazi wenzake katika kampuni ya Apple,lakini hilo halikuwa chaguo rahisi kutangaza hadharani kuhusu jinsia yake.
0 comments:
Post a Comment