Rais Blaise Compaore

Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso amesema atajiuzulu baada ya miezi 12 ya serikali ya mpito.Ameyasema hayo wakati akilihutubia taifa siku moja baada ya kutokea machafuko. Wakati ambao pia Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo ametangaza kuivunja serikali ya nchi hiyo.Katika hotuba yake aliyoitoa kupitia kituo binafsi cha Televisheni, Rais Compaore amesema ameuelewa ujumbe uliotolewa na waandamanaji na kwamba ataondoka madarakani baada ya kumalizika kwa kipindi cha mpito cha miezi miezi kumi na mbili.Wapinzani na waandamanaji nchini humo, waliandamana na kufanya vurugu kupinga kubadilishwa kwa katiba itakayomwongezea muda wa utawala Rais wa nchi hiyo Blaise Compaore, baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka 27.Wamemtaka rais huyo kujiuzulu mara moja.