Friday, May 22, 2015

Friday, May 22, 2015
Mwenyekiti  wa chama cha Tanzania Labour Part (TLP) Agustino Mrema akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uiliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MELEZO ambapo alikanusha  kufukuzwa TLP. Aliyekaa kushoto  ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo na kulia ni Katibu Mkuu wa TLP, Nancy Mrikariya.

MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Agustino Mrema,amesema hajafukuzwa uanachama katika chama hicho.

Mrema aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana kuwa yeye ni mwenyekiti wa Chama hicho na hakuna mtu wa kumtoa kutokana na kuendesha chama hicho kwa kufuata katiba.

Amesema kikundi kinachofanya hivyo na kusambaza taarifa kuwa kimemtoa kutokana na kufanya vikao hakitambui na kuwataka wanachama kuwabeza watu hao. 

Mrema amesema yeye akiwa Mwenyekiti ataendelea kutetea jimbo lake la Vunjo,hivyo watu wanaosema amefukuzwa katika chama wapuuzwe.
Aidha amesema biashara ya Urais ameachana nayo ,sasa kazi yake ni Ubunge kupitia jimbo la Vunjo na ameweza kuleta maendeleo ya wananachi katika jimbo hilo.

0 comments: