Wednesday, June 10, 2015

Wednesday, June 10, 2015
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akipungia mkono maelfu ya wana CCM na wananchi wa Musoma, baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Musoma Juni 9, 2015, kuendelea na kampeni yake ya kuomba wana CCM wamdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015
Lowassa, (kulia), akiwatuliza wana CCM na wananchi wa Musoma, waliojaribu kuvunja geti ili kusalimiana naye alipowasili uwanja wa ndege wa Musoma, Juni 9, 2015, kuomba wana CCM wamdhamini
Wana CCM na wananchi wa Musoma, wakipiga kelele kumwita Mh. Lowassa, ili awasogelee kumsalimia huku wakiwa nje ya geti la uwanja wa ndege wa Musoma
Mh. Lowassa, akiongea na bibi kizee huyu aliyeomba walau amshike mkono ili kumpa baraka katika safari yake ya matumaini 2015, alipowasili kwenye ofisi za CCM wilaya ya Bunda, mkoani Mara, Juni 9, 2015 kuomba wana CCM wamdhamini
Mh. Lowassa, akiwasili ofisi za CCM wilaya ya Bunda
Mh. Lowassa, (kushoto), akiwashukuru wana CCM na wananchi waliojitokeza kwenye ofisi za CCM wilaya ya Bunda, wengine kwa nia ya kumdhamini na wengine kumuona
Umati wa watu uliofurika kwenye ofisi za CCM wilaya ya Bunda, huku wengine wakipanda juu ya mti ili kusuhudia yaliyokuwa yanajiri.

0 comments: