Friday, June 5, 2015

Friday, June 05, 2015
Aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bw.Koffi Annan amemtaka rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kujiuzulu huku uchaguzi mkuu ukiahirishwa.

Kumekuwa na maandamano ya ghasia nchini Burundi pamoja na mapinduzi yaliofeli tangu Nkurunziza atangaze kuwa atawania muhula mwingine wa tatu wa urais katika kile watu wanaamni ni ukiukaji wa katiba.

Annan amesema kwamba rais huyo amepoteza uhalali wake na sasa anafaa kujiuzulu iwapo anawajali raia wa Burundi.
                                    Hali ya maandamano nchini Burundi

Matamshi hayo ya Annan yataongeza shinikizo kwa rais Nkurunziza ,ambaye hadi sasa hajatoa ishara zozote za kujiuzulu.


Uchaguzi wa bunge pamoja na ule wa urais umehairishwa kufuatia wiki za maandamano na ghasia.

Viongozi wa jumuia ya Afrika Mashariki, kwenye kikao chao cha mwisho kilichofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 31/05/2015,walipendekeza uchaguzi wa wabunge na rais uahirishwe kwa wiki sita kufuatia ghasia za kumpinga rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Uchaguzi wa Rais unatarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi Juni

0 comments: