Friday, June 5, 2015

Friday, June 05, 2015
Rais wa Ukraine Bw. Petro Poroshenko , ameonya juu ya kitisho cha kuzuka mapigano makubwa mashariki mwa nchi hiyo, ambako kiasi ya watu 26 wameuwawa katika mapigano mapya  kati ya majeshi ya serikali na waasi wanaoungwa mkono na Urusi, wanaotaka kujitenga.

Mapigano mapya yalizuka karibu na  mgome ya waasi ya Donetsk jana,  miongoni mwa  machafuko makubwa tangu yalipofikiwa makubaliano yakusitisha mapigano yaliotokana na upatanishi wa  Jumuiya ya Ulaya. 

Rais Poroshenko amedai  zaidi ya  wanajeshi 9,000 wa Urusi wako  mashariki mwa Ukraine  kusaidia uasi na kuongeza kwamba Urusi imeendelea kuwapa waasi silaha mpya. 

Umoja wa Ulaya umeelezea wasiwasi wake na kuyaita matukio hayo kuwa ni ukiukaji mkubwa wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliofikiwa mwezi Februari. 

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ameonya juu ya kitisho cha  kupamba moto mapigano.

0 comments: