Friday, June 5, 2015

Friday, June 05, 2015
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, watu wasiojulikana wenye silaha wamelivamia kundi moja la Wairitrea waliokimbilia Sudan kuomba hifadhi na kuwateka nyara watu 14.

 Msemaji wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa, Nicolas Brass amezinukuu mamlaka za Sudan zikisema kuwa, lori la Kamisheni ya Wakimbizi ya Sudan lililokuwa linaelekea kwenye kambi ya wakimbizi ya Shagarab likiwa na watu 49 limeshambuliwa na watu wenye silaha waliokuwa katika gari aina ya pickup.

"Tumejulishwa na mamlaka (za Sudan) kwamba raia wa Eritrea 14 waliokuwa wanaomba hifadhi (nchini Sudan) wametekwa nyara wakati walipokuwa wanaelekea kwenye kambi ya Shagarab kutoka Kassala," iliyoko karibu na mpaka wa Eritrea na Ethiopia, amesema Brass.
Kambi ya Shagarab iko mashariki mwa Sudan na inaendeshwa na serikali ya Sudan kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa na ina watu 15,000 wengi wao wakiwa ni wale walioomba hifadhi.


Taarifa zinasema kuwa hivi sasa kuna raia 110,000 wa Eritrea nchini Sudan, huku maelfu ya Waeritrea wakiingia Sudan kila mwezi kwa tamaa ya kuelekea Ulaya kupitia bahari ya Mediterranean.

0 comments: