Monday, March 16, 2015

Monday, March 16, 2015
                                     

Wafanyabiashara wadogo wanaouza mbogamboga  katika soko la manzese B Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma hasa wanawake wamelalamikia unyanyaswaji wanaodai kufanyiwa na viongozi wa manispaa ya songea kwa kuwaletea askari polisi mara  kwa mara wanaotaka kuwaondoa eneo wanalofanyia biashara kwa nguvu.


Wametoa malalamiko hayo huku wakiwa na watoto wadogo mgongoni  na mizigo ya mboga kichwani baada ya askari polisi kuja eneo wanalofanyia biashara  wakitaka kuwaondoa kwa nguvu eneo hilo na kuwapeleka Dampo la taka ambapo wamemuomba  mkuu wa mkoa wa ruvuma Bw. Said mwambungu kuingilia kati mgogoro huo.
 
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko hilo lililo katika mgogoro  na viongozi wa manispaa ya songea kwa mwaka mmoja sasa Bw.Christian  Mumba  ameuomba uongozi wa manispaa hiyo kukaa nao na kumaliza tatizo hilo.
 
Mkuu wa masoko ya manispaa ya songea Bw.Salumu Homera amesema eneo hilo si mali ya wafanyabiashara bali ni mali ya serikali ambayo inaweza kufanya chochote itakachoamua.

0 comments: