Sunday, November 23, 2014

Sunday, November 23, 2014

Alama za mauaji yaliyotokea Mandera


Makamu wa rais wa Kenya, William Ruto, anasema kuwa askari wa usalama wa Kenya wamewaandama wapiganaji wa al-Shabaab hadi kwenye kambi yao nchini Somalia,baada ya shambulio dhidi ya basi kaskazini-mashariki mwa Kenya hapo jana ambapo raia 28 wa Kenya waliuawa na wapiganaji wa kikundi hicho kwa kupigwa risasi vichwani.
Bwana Ruto alisema wapiganaji zaidi ya 100 waliuliwa katika operesheni mbili tofauti.
Alisema kambi ya al-Shabaab iliangamizwa.
Habari hizo hazikuthibitishwa na upande wa pili.
Gavana wa Mandera - ambako shambulio la jana lilitokea - amelaumu vikosi vya usalama kwa kushindwa kuwalinda raia.
Alisema polisi kawaida wanashindwa kufanya uchunguzi kamili baada ya mashambulio.

0 comments: