Mhubiri maarufu wa Bahamas Faith Ministries Dr.Myles Munroe amefariki Dunia kwenye ajali ya ndege aliyokuwa Amepanda.
Ajali hiyo imetokea siku ya Jumapili wakati akiwa ndani ya ndege
ambayo Amepanda inaelezwa kuwa Iligonga kifaa kinachonyanyua vitu vizito
wakati wa ujenzi na kulipuka nchini Bahamas.
Munroe na mkewe, Ruth, walikuwa miongoni mwa waathiriwa 9 kwenye
ajali hiyo kwenye iliyotokea kwenye uwanja wa ndege wa Grand Bahama,
Bahamas Tribune limebaini.
Ndege ndogo ilipata ajali baada ya kugonga kifaa hiko wakati
ikikaribia kutua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Grand Bahama,
kwa mujibu wa maafisa.
Duru za habari BFMI zinasema kuwa ,Munroe anayejulikana kimataifa alikuwa Rais wa Myles Munroe International (MMI).
BFMI umemueleza Munroe kuwa alikuwa “Mhadhiri, mwalimu, kocha wa
maisha, mshauri wa serikali na mshauri wa uongozi,”Ndege hiyo ilipata
ajali wakati watu wamejikusanya katika Grand Bahama kwa ajili ya Global
Leadership Forum- tukio lilliloandaliwa na Munroe.
0 comments:
Post a Comment