Vuguvugu
la uchaguzi wa serikali za mitaa limeanza kutanda katika maeneo
mbalimbali ya jiji la Arusha huku chama cha Demokrasia na maendeleo
(Chadema) kikiitaka serikali na idara zinazohusika kuwadhibiti watu
wanaoanza kuwapotosha wanachi kupitia mitandao ya kijamii.
Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha Bw. Kalst Lazaro amesema wakati
muda wa uchaguzi ukiendelea kukaribia baadhi ya mambo yanayoweza
kuleta malumbano yasiyo ya msingi yameanza kujitokeza likiwemo la
baadhi ya watendaji kupotosha na kuwachanganya wananchi juu ya
daftari la wapiga kura na daftari la wakazi.
Wakizungumzia tatizo hilo baadhi ya madiwani wa Chadema na pia wa
chama cha mapinduzi wamekiri kupokea malalamiko ya mkanganyiko wa
madaftari hayo na pia kuwepo kwa watu wanaoanza kuwapotosha wananchi na
licha ya kuwataka wananchi kuwapuuza wamezitaka idara zinazohusika
kuwadhibiti watu hao kabla hawajaleta madhara.
Arusha ni miongoni mwa mikoa yenye upinzani mkubwa wa kisiasa na
ambayo ina historia ya kuwa na heka kubwa wakati wa uchaguzi ambazo
wakati mwingineimekuwa ikisababisha vurugu zinazopelekea watu
kujeruhiwa na hata kupoteza maisha.
0 comments:
Post a Comment