Sunday, February 22, 2015

Sunday, February 22, 2015
Kiungo wa zamani wa Simba na Timu ya taifa, Christopher Alex Masawe
                              
MWENYEZI Mungu ailaze roho ya kiungo fundi wa zamani wa Simba, Christopher Alex Masawe.
Alex amefariki dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya Milembe, mkoani Morogoro.
Nyota huyu aliyepiga penalti ya mwisho mwaka 2003 Simba ikiwavua ubingwa wa Africa, Zamalek ya Misri amesumbuliwa na maradhi ya muda mrefu.
Mama mzazi wa Alex amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.
Alex alikuwa anaishi na mama yake ambaye alikosa uwezo wa kumuuguza na mara kadhaa alikuwa anaomba msaada kwa wasamaria wema wakiwemo wadau wa Soka.
Uongozi wa Simba haukuwahi kumpa msaada mkubwa Alex, licha ya kundi la mashabiki na wanachama kumchangia kiasi kidogo cha fedha.
Pia mashabiki wa klabu ya jamii ya Mbeya City walifika mkoani Dodoma wakisafiri kwenda Mwanza ambapo Mbeya City ilicheza na Kagera Sugar na wakamchangia laki mbili na ushee.

0 comments: