Zaidi ya maduka 90 ya biashara yaliyoko pembezoni mwa shule ya sekondari ya pamba jijini mwanza yamefungwa kwa amri ya mkurugenzi wa jiji la mwanza baada ya wawekezaji watatu waliopewa zabuni ya ujenzi wa maduka hayo kushindwa kulipa deni la shilingi milioni 445 kwa bodi ya Shule ya Sekondari Pamba.
Zoezi la kufunga maduka hayo limeongozwa na kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Tito Mainya kwa kushirikiana na askari mgambo wa jiji.
Wawekezaji hao ambao maduka yao yamepigwa kufuli ni Albert Swai ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Hilgo Construction Ltd anayemiliki maduka 25 anadaiwa deni la shilingi milioni 88 na mia nne pamoja na mkurugenzi wa kampuni ya Lewico, Wilson Christopher mwenye maduka 65 akidaiwa shilingi milioni mia tatu hamsini na saba na laki tano. Fedha hiyo ni sawa na asilimia 25 ya makusanyo ya kila mwaka toka kwa wawekezaji hao.
Baadhi ya wafanyabiashara waliopangishwa kwenye vyumba hivyo vya maduka yaliyopigwa kufuli, vinavyomikikliwa na Albert Swai wa kampuni ya Hilgo pamoja na Wilson Christopher wa kampuni ya Lewico wamelalamikia hatua hiyo.
0 comments:
Post a Comment