Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof.Jakaya Mrisho Kikwete amesema miradi mingi ya maendeleo inayotegemea misaada ya kisayansi kutoka katika nchi zilizoendelea hukwama kwa nchi hizo kusitisha misaada pale nchi masikini tanzania ikiwemo zinapokataa kutekeleza matakwa ya nchi hizo hivyo ni vyema nchi masikiini zikawa na mkakati maalum wa kuanza kuwekeza katika nyanja za kisayansi.
Rais Kikwete ameitoa kauli hiyo jijini Dar es salaam, katika harambee ya kuchangia ujenzi wa chuo kikuu cha Tumaini kampasi ya Dar es salaam na kuongeza kuwa taifa lolote linalotegemea misaada kutokanje ya nchi haliwezi kuwa na maendeleo endelevu kwani nchi masikini zinapotofautiana na matakwa ya nchi zinazotoa misaada hususan ya kisayansi husitisha misaada yao na hivyo kukwamisha maendeleo ya nchi husika.
Rais Kikwete amezitaka taasisi na vyuo vikuu vya hapa nchini kuendelea kuimarisha miundo mbinu ya kujifunzia hususani ya kisayansi ili kuondokana na kadhia ya kutegemea misaada ya kisayansi kutoka katika nchi zilizoendelea kwa kuwekeza katika sekta ya elimu ili kupata wataalam watakaosaidia maendeleo ya nchi.
Kwa upande wake askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT, Askofu Alex Malasusa ameishukuru serikali kwa jitihada zake za kusaidia wananchi wa hali ya chini ili waweze kupata elimu ya juu kwa kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wote wenye sifa na kwamba kanisa hilo litajitahidi kuendelea kuchangia katika sekta ya elimu kupitia taasisi zake za elimu.
0 comments:
Post a Comment