Monday, March 2, 2015

Monday, March 02, 2015
SAMSUNG CSC
Madaktari Bingwa (waliokaa viti vya mbele kushoto) kutoka Hosptali ya Taifa Muhimbili na Taasisi y mifupa (MOI) wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo pichani) katika uzinduzi wa huduma za Kitaalam katika Hospitali ya Kitete leo.



ya   SAMSUNG CSCMjumbe wa Bodi ya NHIF, Bw. Charles Kajege akitoa ufafanuzi wa taratibu za huduma kwa wanachama wa Mfuko huo muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa zoezi la madaktari bingwa.

SAMSUNG CSC
Wananchi wakifuatlia hotuba kwa makini

SAMSUNG CSC
Wananchi wa Mkoa wa Tabora waliohudhuria uzinduzi huo.

SAMSUNG CSC 
Wananchi wakiwa na hamu ya kukutana na Madaktari Bingwa

nh7
         
Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma, Grace Michael akifurahia jambo na madaktari bingwa katika uzinduzi wa huduma hizo.

Wananchi wa Mkoa wa Tabora wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Bw. Rudovick Mwananzila, wamesema kuwa kitendo kilichofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya cha kuwapelekea Madaktari Bingwa katika mkoa huo ni faraja kwao lakini pia kimeonesha namna wanavyothamini wananchi na wanachama wao.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Madaktari Bingwa katika Hospitali ya Mkoa huo, Kitete, Bw. Mwananzila aliupongeza uongozi wa NHIF kwa uboreshaji wa huduma wanaoufanya ambao sasa unawafikia wananchi wote bila kujali umbali wa mikoa hiyo.
“Kitendo hiki kimekuwa faraja sana kwetu, ninayo furaha kubwa kuwapokea madaktari hawa ambao naamini watatoa huduma kwa wananchi wenye mahitaji ya utaalam wao, lakini imepunguza mzigo kwa wahitaji ambao uwezo wa kwenda Muhimbili au Bugando ni mdogo…kwa kifupi NHIF kweli mnafanya kazi kwa kutanguliza maslahi ya wananchi wa Tanzania,” alisema Bw. Mwananzila.
Aidha alitumia mwanya huo kuushukuru Mfuko pia kwa kutoa dawa na Vifaa tiba vitakavyotumika katika zoezi hilo na kuuagiza uongozi wa Hospitali kuhakikisha msaada huo unatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Akizungumzia huduma za matibabu kwa ujumla, Mkuu huyo wa Mkoa alikemea tabia zinazofanywa na baadhi ya watumishi wa sekta ya afya kutanguliza mbele maslahi yao badala ya kuzingatia miongozo na maadili yao ya kazi.
“Niwaambie tu kwamba mie sitamuonea aibu mtumishi yoyote wa Hospitali ambaye ataonekana ananyanyasa au kuwasumbua wanachama wa NHIF na Mfuko wa Afya ya Jamii kwani vitendo hivi vinakwamisha juhudi za Serikali hususan suala la wananchi kujiunga na Mifuko hii,” alisema Bw. Mwananzila.
Kwa upande wa Mjumbe wa Bodi ya NHIF, Bw. Charles Kajege alisema kuwa utaratibu wa kupeleka Madaktari Bingwa katika mikoa ya pembezoni ni endelevu kutokana na mazingira pamoja na mahitaji ya wananchi wa maeneo hayo.
“Sisi kama Bodi, tutaendelea kuhakikisha huduma hizi zinawafikia wananchi wote bila kujali mazingira wanayoishi kwa kuwa lengo letu ni kuona huduma zinakuwa bora lakini pia wanachama na wananchi wananufaika na Mfuko huu,” alisema.
Kutokana na hali hiyo aliwataka wananchi wa Mkoa wa Tabora na maeneo ya jirani kuhakikisha wanatumia fursa hiyo vizuri ili waepukane na upotevu wa fedha nyingi na muda kwa ajili ya kufuata huduma hizo za kitaalam ambazo Mfuko imezisogeza.

0 comments: