Sunday, March 8, 2015

Sunday, March 08, 2015
                                        Raia wa Israel wakifanya maandamano ya kupinga uongozi wa Netanyahu

Watu zaidi ya 25 elfu wameshiriki kwenye mhadhara mjini Tel Aviv, kumpinga waziri mkuu, Benjamin Netanyahu ambapo walitaka mabadiliko katika mwelekeo wa siasa na uongozi wa Israel.

Meir Dagan, mkuu wa zamani wa shirika la ujasusi la Israel, Mossad, ameuambia mkusanyiko huo jana usiku, kuwa uongozi wa nchi hiyo unamtisha zaidi, kuliko anavyotishwa na maadui.

                           Waziri Mkuu wa Israeli,Benjamin Netanyahu




Mhadhara huo ulitayarishwa na shirika la raia, linalotaka makubaliano ya amani baina ya Israeli na Wapalestina.
Waandishi wa habari wanasema hayo yalikuwa kati ya maandamano makubwa kabisa dhidi ya serikali, kufanywa kabla ya uchaguzi wa kati ya mwezi.
Hivi karibuni, katika ziara yake nchini Marekani, Bw.Netanyahu alilihutubia baraza la Congress na kuelezea azma yaka ya kutoiona Iran ikitekeleza mradi wake wa nyuklia. Hata hivyo, msimamo wake huo ulipingwa kwa uwazi saa chache baadae na rais wa Marekani, Barack Obama kwa kusema kuwa haukutoa njia mbadala na yenye utatuzi kwa namna ya kumaliza mpango wa nyuklia wa Irani. Iran iliita hotuba ya Bw. Netanyahu kuwa ya kuudhi kama zinavyokuwa hotuba zake nyingine.

0 comments: