Sunday, March 8, 2015

Sunday, March 08, 2015
Simba wanamaliza mpira kwa kupiga pasi zaidi ya 28 bila ya kupoteza hadi mwamuzi Martin Saanya alipomaliza mpira
Dk 90+3


Dk 89, Maguri anapiga kichwa safi mbele ya mabeki wa Yanga na Barthez anafanya kazi nzuri na kuokoa.



Dk 88, anatoka Abdi banda na nafasi yake inachukuliwa na Simon Sserunkuma.

Dk 87 Yanga wanapata kona baada ya shambulizi langoni mwa Simba

Dk 84, cannavaro anacheza vizuri na kumzuia Messi aliyepigiwa pasi nzuri na Okwi


Dk 80, Okwi anapiga shuti jingine kali lakini linapita juu kidogo ya lango la Yanga


Dk 79, Msuva anapiga faulo vizuri lakini mpira unaokolewa vizuri na Ivo anayeruka juu na kupangua

Dk 77 anatoka Ngassa nafasi yake inachukuliwa na Kpah Sherman

Dk 75, Simba wanamtoa Ibrahim Ajibu anaingia Elius Maguri.

KADI NYEKUNDU Dk 74: Niyonzima anapewa kadi ya pili ya njano inayozaa nyekundu. Alifanya kosa la kuupiga mpira kwenye nyavu za Simba baada ya mwamuzi Saanya kuwa amepuliza filimbi lakini yeye akaubutua mpira.

Dk 70, Javu anamtoka Kessy na kupiga shuti kali ambalo Ivo analiokoa.

Dk 62 hadi 64, kidogo ni mpira unakuwa wa matukio, wachezaji wanasukumana, Okwi anafanyiwa madhambi na Twite, anatolewa nje kutibiwa na huko inaonekana Kpah Sherman anainuka na kuanza kupasha.

Dk 61, Ajibu anapata nafasi nzuri katika ya lango la Yanga baada ya mabeki wa Yanga kugongana lakini 'anaichezea' kwa kupiga shuti kubwaaa!

Dk 60 Yanga wanapata kona lakini Simba waokoa kwa ulahisi


Dk 53 hadi 56 mpira zaidi unachezwa katikati huku Yanga wakionekana kupania zaidi.


GOOOOOOOOO Dk 52, Okwi anaifungia Simba bao baada ya kumchungulia Barthez aliyekuwa mbele ya lango na kupiga mpira mrefu unaojaa moja kwa moja nyavuni.

KADI Dk 49 Nadir Haroub 'Cannavaro' analambwa kadi ya njano kwa kumkata Ibrahim Ajib

DK 47 Yanga wanaingia vizuri katika eneo la hatari la Simba, Tambwe anashindwa kuuwahi mpira, Murishid anaondosha


MAPUMZIKO:
DK 45 Tambwe anaweka kifuani vizuri anamuachia Msuva lakini anapaisha juu

DK 43 anapiga faulo Okwi inatoka kidogo nje ya lango la Yanga

KADI Dk 42, Niyonzima anamuangusha Singano na kupewa kadi ya njano

Dk 41, Tambwe anaingia katika eneo la  hatari la Simba na kupiga shuti lakini linatua kwa ulaini katika mikono ya Ivo Mapunda.

Dk 36, Ivo anaokoa mpira miguuni mwa Ngassa anabaki Msuva peke yake na mpira anashindwa kulenga lango.

KADI 34 Saanya anatoa kadi za Njano kwa Banda na Yondani

MABADILIKO :DK 30, Yanga wanamtoa DANNY MRWANDA na HUSSEIN JAVU anachukua nafasi yake

Dk 27 Singano anagongana na kipa Barthez, sasa anatibiwa...


Dk 24, Mrwanda na Kessy wanalambwa kadi za njano kutokana na faulo na kuchezeana kibabe.


Dk 21, Mwamuzi Said Juma Makapu analambwa kadi ya njano.

Dk 19, Tambwe anapiga kichwa mbele ya Murishid na mpira unapita juu ya lango la Simba


Dk 18, Msuva anaingia vizuri ndani ya eneo la 18 ya Yanga, lakini Murishid anaokoa.

Dk 14, Cannavaro anamuangusha Okwi aliyekuwa anakwenda langoni mwa Yanga lakini faulo aliyopiga Okwi inaishia miguuni mwa wachezaji wa Yanga.


Dk 9, Yondani anafanya kazi ya ziada kumzuia Okwi na kuondoa mpira huo.

Dk 8, Msuva anaingia kwa kasi, anamzidi mbio Mohammd Hussein na kupiga shuti dhaifu.


Dk 2, Ibrahim Ajib anakuwa wa kwanza kupiga shuti kali lakini linapita pembeni mwa lango la Yanga.


Dk 1 Mechi imeanza kwa kasi na Yanga wanakuwa wa kwanza kupata kona, lakini haina matunda.

0 comments: